Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi (SACP), Fortunatus Muslim, (watatu kutoka kulia) akiongea wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupima ulevi kwa madereva vilivyotolewa na TBL Group katika maadhimisho ya Siku ya Unywaji bia kistaarabu,mwishoni mwa wiki, wengine pichani (wa nne kutoka kulia ) ni Afisa Mawasiliano wa TBL, Amanda Walter na Maofisa wengine kutoka Jeshi la Polisi.
3.Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda Walter akiongea wakati wa hafla hiyo.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi (SACP), Fortunatus Muslim katika picha ya pamoja na askari waliohudhuria hafla hiyo pamoja na Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter.
KAMPUNI ya Tanzania Breweries Limited (TBL Group), chini ya kampuni mama ya ABInBev, mwishoni mwishoni mwa wiki iliadhimisha siku ya Unywaji wa Pombe Kistaarabu diniani kwa kushiriki kampeni mbalimbali za kuhamashisha matumizi ya vinywaji vizuri kwenye jamii.
Mbali na uhamasishaji huo uliofanyika katika mikoa mbalimbali nchini ambako kampuni inaendesha biashara zake pia kampuni ilitoa vifaa vya kupima kiwango cha ulevi kwa madereva kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani.
Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika hafla iliyofanika mwishoni mwa wiki,Afisa Mawasiliano wa TBL, Amanda Walter alisema kuwa kupitia sera ya kampuni ya Smart Drinking Goals,siku zote itahakikisha inahamasisha matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kiafya na burudani na sio kuleta athari kwa jamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.