ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 14, 2018

MAREKANI:- VIKWAZO DHIDI YA ZIMBABWE VITAENDELEA KUWEPO.

Marekani: Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vitaendelea kuwepo
Manisha Singh.
Serikali ya Marekani haitaondoa vikwazo ilivyoiwekea Zimbabwe hadi pale serikali mpya ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo itakapodhihirisha kuwa inabadili mielekeo yake. Hayo yameelezwa na afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya uchumi wa Marekani.
Naibu Waziri wa Uchumi na Masuala ya Biashara wa Marekani, Manisha Singh amesema kuwa watu na taasisi 141 za Zimbabwe akiwemo Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe wako chini ya vikwazo vya Marekani.  Amesema mashinikizo ya Marekani kwa Zimbabwe bado yako palepale.

Amedai kuwa Washington inajaribu kutumia njia ya mashinikizo ili kushawishi mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na kuheshimiwa haki za binadamu. Naibu Waziri wa Uchumi na Masuala ya Biashara wa Marekani ameongeza kuwa Washington itaanzisha tena uhusiano wa kawaida na Zimbabwe baada ya kushuhudia mabadiliko ya msingi nchini humo. 
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe.
Mnangagwa ametoa wito wa kuondolewa vikwazo hivyo vya Marekani dhidi ya maafisa wa chama tawala Zanu-pf, maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi na baadhi ya mashirika yanayomilikiwa na serikali vilivyowekwa wakati wa utawala wa Mugabe kwa sababu ya kile ilichokitaja kuwa ni ukiukaji wa haki za binadamu na demokrasia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.