ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 15, 2018

MKUU WA WILAYA MISUNGWI AGOMA KUKABIDHI PIKIPIKI KWA AFISA ELIMU KATA KISA MIMBA ZA WANAFUNZI


NA GSENGOtV

MKUU wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda ameahirisha zoezi la kukabidhi pikipiki kwa Afisa Elimu kata ya Igokelo Baraka Dede Japhet  kufuatia shutuma zinazotajwa dhidi yake kuwalea na kuwakingia kifua watu wanaotajwa kuwapa mimba watoto wa shule za kata yake. 

Kwa wilaya ya Misungwi kata ya Igokelo inatajwa kuongoza kwa  vitendo vya wanafunzi kupata ujauzito wakiwa mashuleni hali inayosababisha wanafunzi hao kukatisha masomo.

Kwa upande wake Afisa huyo amejitetea kwa kusema kuwa hatua zote stahiki zilikuwa zikichukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwakama watuhumiwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

"Hata walionaswa jana, tumewakamata na kuwaripoti kwa vyombo vya dola na  taarifa zao tumeziandikia taarifa, tulikuwa na mtendaji wa kata lakini nashangaa kuambiwa kwamba sichukuwi hatua" alisema Dede

Ili kuwaondolea adha ya usafiri na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ilikabidhi pikipiki 180 kwa kata mbalimbali za mkoa wa Mwanza, ambapo kwa wilaya ya Misungwi, pikipiki 26 zimekabidhiwa kwa maafisa hao huku pikipiki moja ikisalia kufanya idadi ya pikipiki 27 kwa kata hiyo yenye changamoto, mpaka pale uchunguzi utakapo kamilika. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.