Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imepiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi kwenda wilaya nyingine kwa lengo la kuchenjuliwa.
Akzungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza Juma Sweda alipiga marufuku na kuwataka madiwani na watendaji kusimamia kikamilifu utekelezaji wake.
Alisema lengo la kuzuia usafirishaji wa madini ghafi hayo ikiwemo dhahabu na chuma ni kuhakikisha uchenjuaji unafanyikia ndani ya wilaya ya Misungwi ili kuongeza fursa ya ajira kwa wananchi pamoja na ukusanyaji mapato.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Kisena Mabuba alisema zuio hilo litasaidia kudhibiti mapato yanayopatikana kutokana na shughuli za uchenjuaji madini hivyo atashirikiana vyema na watendaji wake ili kutekeleza vyema zuio hilo.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Antony Bahebe aliwataka madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la asilimia 100 mwaka 2018/19 kutoka asilimia 80.16 mwaka 2017/18 huku wakihakikisha hakuna upotevu wa mapato ya halmashauri hiyo na kwamba watakaoshindwa kufanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.