ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 1, 2018

MAKONTENA YA MAKONDA YAKOSA WATEJA TENA.


MNADA wa makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, umefanyika leo Jumamosi, Septemba 1, 2018 katika Bandari ya Dar, lakini imeshindikana kupatikana mnunuzi, hivyo mnada huo utaendelea Jumamosi ijayo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Scolastika Kevala, amesema hawajapata mnunuzi wa kontena hata moja lakini wamefanikiwa kuuza bidhaa 10 tu zilizokuwemo kwenye makontena hayo.

Sehemu kubwa ya bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama vile viti, meza na makabati na vitu vingine.

“Mpaka sasa tayari tumefanya mnada wa makontena yote 20 lakini hayajapata mteja ingawa tumefanikiwa kuuza bidhaa 10 zilizokuwemo kwenye makontena hayo. Hivyo mnada wa makontena utaendelea tena Jumamosi ijayo,” amesema Kevela.

Itakumbukwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango aliagiza makontena hayo kupigwa mnada licha ya RC Makonda kutoa vitisho kuwa atakayenunua vitu vilivyomo kwenye makontena hayo atapata laana.

Aidha, mnada wa makontena hayo unakuja ikiwa ni baada ya Makonda kushindwa kuyalipia kodi kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.