ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 30, 2018

MCHEZAJI BORA ULAYA KUJULIKANA LEO.GSENGOtV
Tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa Ulaya (UEFA) msimu wa 2017/18 inatarajiwa kutolewa usiku wa leo mjini Monaco nchini Ufaransa ambapo majina matatu yanayowania tuzo hiyo ni Cristiano Ronaldo wa Juventus, Mohamed Salah anayechezea Liverpool na Luka Modric wa Real Madrid.

Tuzo hiyo imevuta hisia kubwa ya mashabiki wa soka kutokana na namna kila mchezaji alivyopambana kuisaidia klabu yake kwa msimu mzima uliomalizika. Hapa tunakuletea uchambuzi wa kila mchezaji kuelekea tuzo hiyo.

Cristiano Ronaldo, mshindi huyo mara tano wa BallonD’or na tuzo ya mfungaji wa goli bora la msimu uliopita wa klabu bingwa ulaya licha ya kutofanya vizuri na Real Madrid katika Laliga, aliisaidia kwa kiasi kikubwa kushinda taji la 13 la klabu bingwa ulaya huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake 15 likiwemo bao lake katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Juventus lililoshinda tuzo ya goli bora la msimu la klabu bingwa ulaya.

Rekodi kadhaa alizoweka msimu uliopita ikiwemo kuwa ni mchezaji wa kwanza kufunga bao katika mechi 11 mfululizo za klabu bingwa ulaya pamoja na kushinda tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya sita mfululizo na kuisaidia kushinda ubingwa mbele ya Liverpool, inamfanya kuwa ni mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo katika usiku wa leo.

Mohamed Salah, alikuwa na msimu bora sana ambao wengi hawakutarajia kutokana na alichokifanya, alifunga jumla ya mabao 44 katika mashindano yote akilingana na Cristiano Ronaldo huku akiwa nyuma ya Lionel Messi ambaye alifunga mabao 45 na kuisaidia Liverpool kucheza fainali dhidi ya Real Madrid ambayo aliumia katika mchezo huo na kushuhudia Liverpool ikipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

Pia alishinda tuzo ya (PFA) mchezaji bora wa EPL pamoja na kiatu cha dhahabu kwa mabao yake 32 katika ligi hiyo. Tuzo zingine alizoshinda ni mchezaji bora wa mwaka barani Afrika, tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika na kumfanya kuwa ni mchezaji anayepewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo kwa mara yake ya kwanza.

Luka Modric, kiungo huyo ameng’ara katika michuano ya klabu bingwa ulaya akiwa na Real Madrid na kuisaidia kushinda ubingwa, pia alionesha kiwango kikubwa katika michuano ya kombe la dunia na kuiongoza timu yake ya taifa ya Croatia kufika fainali ya michuano hiyo licha ya kupoteza kwa mabao 4-2. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika michuano hiyo ya kombe la dunia na kuandikisha historia kwa nchi yao kufika hatua hiyo kubwa katika kombe la dunia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.