NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Baraza la vetenari nchini limeyafunga maduka kumi
ya pembejeo za mifugo jijini mwanza baada ya kubaini kuwa maduka hayo hayana
leseni ya kufanya biashara ya kuuza pembejeo pamoja na kutokuwa na wataalam wa
mifugo.
Mkaguzi wa baraza hilo DKT.GEORGE MTINDA amesema
kuwa wamiliki wa maduka yaliyofungiwa watalazimika kulipa faini pamoja na
kuajiri wataalam wa mifugo ili yaweze kuendelea na biashara ya pembejeo.
Katika msako huo, Baraza hilo limebaini maduka 10
ambayo hayana wataalam wa mifugo na leseni za kuendesha biashara ya dawa za
mifugo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.