Rais John Magufuli amesema hajapendezwa na utendaji kazi wa uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutokana na wizara hiyo kufanya mambo ya ovyo.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 2, 2018 Ikulu Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua akiwemo Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
Amesema ukiondoa kazi zinazofanywa na makamishna, hajapendezwa na utendaji wa uongozi wa juu.
“Nakupeleka pale ukafanye kazi na wewe bahati nzuri ni askari. Nilifanya uchunguzi wa miradi ya polisi katika vituo 108, palikuwa na mkataba wa Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na mtu anaitwa Lugumi wa Sh37bilioni,” amesema.
“Tulipewa maagizo kama Serikali tuyashughulikie na tuyatafutie ufumbuzi lakini mpaka leo hii haijapatiwa ufumbuzi,”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.