ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 2, 2018

MWENYEKITI UVCCM HERY JAMES, ATOA DARASA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU 30 MKOANI MWANZA

 NA ZEPHANIA MANDIA GSENGOtV.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama chamapinduzi (UVCCM) taifa KHERI JAMES amewataka vijana wasomi nchini kuwa wazalendo na kutumia  elimu yao kusaidia jamii inayowazunguka kwa kutatua changamoto zinazowakabili hasa elimu.

Akizungumza wakati mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati mkoani mwanza,JAMES amesema umuhimu wa elimu hususani kwa vijana itaonekana ikiwa changamoto za jamii zitapatiwa ufumbuzi aidha amewahimiza wasomi nchini kubuni miradi ya kuwaingizia vipato ili kupunguza tatizo la ajira miongoni mwa vijana.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM taifa amelazimika kutoa rai hiyo baada ya  katibu wa shirikisho hilo  SELEMAN BARUAN kuomba kupatiwa ajira katika serikali pamoja na chama chamapinduzi pamoja na jumuiya zake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.