GSENGOtV
Katika kupambana na ujambazi jijini Mwanza Jeshi la Polisi mkoani humo limefanikiwa kumuua jambazi anayefahamika kwa jina la Seleman Israel (54) aliyekuwa akijaribu kuwakimbia polisi huku mmoja jina lake Salvatory Emanuel(45) akifanikiwa kutoroka.
Watuhumiwa hao wa ujambazi walikamatwa alfajiri ya leo Julai 24,2018 maeneo ya Luchelele Wilayani Nyamagana wakijihusisha na ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo ya pembezoni mwa Wilaya ya Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza.
Katika mahojiano na jeshi la Polisi watuhumiwa walikiri kujihusisha na ujambazi kwa kutumia silaha na wanayo silaha wanayotumia katika uhalifu na wameificha maeneo ya Luchelele.
Pamoja na hayo wamekiri kuwa walihusika na mauaji ya mlinzi wa lindo maeneo ya Igombe mkoani humo.
Baada ya mahojiano hayo watuhumiwa hao wa ujambazi waliongozana na Polisi hadi eneo waliloficha hiyo silaha hiyo na mara baada ya kufika ghafla majambazi hao walikurupuka na kuanza kukimbia,polisi walijaribu kupiga risasi hewani na kuwaamuru wasimame lakini walikaidi amri hiyo hivyo polisi walipiga risasi zingine na kufanikiwa kumlenga jambazi huyo mmoja maeneo ya kiunoni huku mmoja akifanikiwa kuwatoroka polisi,jambazi huyo amefariki wakati ankipelekwa hospitali kwa matibabu.
Aidha, baada ya Polisi kufika eneo lililodaiwa kufichwa silaha polisi walikuta silaha aina ya Ngobore,risasi nne za AK47, risasi tano za maganda mawili ya RIFLE, kipande cha nondo, panga tatu na vifaa vingine vinavyotumika katika uvunjaji.
Jeshi la polisi linaendelea na msako wa kumpata jambazi aliyetoroka na wengine wanaoshirikiana nao kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Mwanza.
Mwili umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi na pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishna wa polisi Ahmed Msangi anatoa onyo kwa wakazi wa Mwanza hususani vijana akiwataka kuacha tabia ya kujihusisha na uhalifu na kuwasisitiza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kukomesha vitendo vya uhalifu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.