Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, na viongozi wengine wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA Awamu ya Tatu (REAIII), kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Julai 9, 2018. Mhe. Naibu Waziri pia alitumia fursa hiyo kusikilzia kero za wnanchi kuhusu upatikanaji umeme kwenye vijiji vyao.
NA
K-VIS BLOG, MOROGORO
NAIBU
Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, amezindua mradi wa usambazaji umeme
vijini REA awamu ya tatu (REAIII), ambapo jumla ya vijiji 180 vya Mkoa wa
Morogoro vitanufaika.
Naibu
Waziri alifanya uzinduzi huo kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani
humo Jumatatu Julai 9, 2018 kwa kukata utepe na kuwasha swichi ya umeme na hivyo kuibua shangwe, nderemo na vifijo kutoka
kwa wananchi waliojawa na furaha.
Akizungumza
baada ya uzinduzi huo Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu, alisema, Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli inayo dhamira ya kweli ya kuhakikisha ahadi zote
ilizotoa kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wote wa Tanzania mijini
na vijijini inatekelezwa kwa kasi.
“Tayari umeme umefika sasa utumieni kika
milifu kujiletea maendeleo yenu na taifa kwa ujumla.” Alisema Mhe. Naibu
Waziri.
Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni
nafuu sana kiasi cha shilinbgi Elfu Ishoirini na Saba tu (27,000)
Wananchi wakimsikilzia Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakayti akihutubia
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa
Diwani
wa kata ya Kimamba A, Upendo Mpoto akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa
Nishati, Mhe. Subira Mgalu wakati akisikiliza kero zinazohusiana na mradi wa
umeme vijijijini.
Diwani wa Kata ya Kimamba akizungumza kwenye mkutano huo. |
Naibu
Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (Mwenye Kilemba chekundu kichwani)
akimsikiliza Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Bw. Stephen
Lukobe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maful. Wakwanza
kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Maganga.
Naibu
Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu kulia akizungumza jambo na Diwani wa kata
ya Kitete wilaya ya Kilosa, Stephen Lukobe katika ofisi ya kijiji cha Madudu
wakati wa ziara ya naibu waziri huyo ya kutembelea vijiji vitavyonufaika na
mradi wa umeme wa REA Awamu ya tatu (REAIII), mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro
Julai 9, 2018
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.