ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 10, 2018

TUWE WAWAZI UGONJWA WA KIPINDUPINDU UNASABABISHWA NA UCHAFUGSENGOtV
DR. Sebastian Ndege Mkurugenzi wa Jembe Media Group hapa anafafanua kuhusu namna ugonjwa wa kipindupindu unavoingia kwa mwanadamu ni wakati alipofanya mahojiano na kipindi cha Kazi na Ngoma ya Jembe Fm Mwanza.KIPINDUPINDU: DALILI, TIBA NA NAMNA YA KUJIKINGA.


Kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na aina ya bakteria aitwaye Vibrio cholerae, Ugonjwa huu ni wa kuambukizwa kwa njia ya viini vinavyoenezwa kupitia kwa kinyesi kutoka kwa wagonjwa wenye Kipindupindu.

Kipindupindu sana sana iwapo mahali hakuna maji ya mfereji au mabomba ya kupitisha maji machafu.

Mabomba ya kupitisha maji machafu yasiyofunikwa na matanki ya maji ya kunywa yasiyofunikwa huchangia katika kusababisha mkurupuko wa kipindupindu.

Kwa sababu hii, ugonjwa wa kipindupindu ni shida inayotokea sana sehemu za mashambani au vitongoji duni kwenye hakuna maji ya mfereji na mabomba ya maji machafu.

 

Bakteria aenezaye ugonjwa wa Kipindupindu

Dalili

1. Dalili bainifu ya ugonjwa huwa ni kuharisha sana haja iliyo majimaji.

2. Mwili hushindwa kutumia maji na chakula hivyo basi kumfanya mgonjwa kudhoofika haraka kwa sababu ya kukosa maji mwilini.

3. Mgonjwa huhisi kiu kingi na uchovu mwingi, na hushindwa kutulia.

4. Ngozi ya nje na ndani itanyauka na macho yataingia ndani na watahisi kichefuchefu na kiharusi kisicho cha kawaida.

Vipimo
Madaktari huchukuwa choo cha mtu kuangalia iwapo ana kipindupindu, kwani viini vyake havipatikani kwa damu.

Matibabu


1. Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya.

2. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.

3. Chanjo za kuzuia Kipindipindu ambazo hutolewa katika baadhi za nchi.Kuepukana na Kipindupindu
Kinga ni kama ifuatavyo:

 • Wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama sahani, vikombe n.k.
 • Nawa mikono kabisa kwa sabuni – kiganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha kwa sekunde. Baada ya haja na kabla ya kula.
 • Kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
 • Kupika chakula vizuri maana halijoto juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria;
 • Kumenya matunda yote
 • Kufunika chakula maana nzi wanapitisha bakteria kwa miguu yao
 • Maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia mashimo ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria
 • Vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto
 • Mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao inapaswa kunaniwa kwa sabuni
 • Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia klorini
 • Tumia maji yaliyotibiwa pekee hasa ikiwa ni ya kunywa; yachemshe au utie matone 5 ya klorini kwa kila galoni 1 au utumie dawa ya kutakasa maji. Yaache maji yatulie kwa dakika 30 kabla ya kunywa.
 • Tumia choo kila mara – usiende haja karibu au ndani ya chanzo cha maji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.