Mwanamasumbwi maarufu duniani kutoka Marekani, Floyd Mayweather ameamua kuliamsha bifu na swahiba wake wa zamani 50 Cent hii ni baada ya rapper huyo kumuandamana Mayweather kwenye mitandao ya kijamii.
Mayweather akitema nyongo kwenye ukurasa wake wa Instagram amefunguka kuwa 50 Cent kwa sasa anahasira na kila kijana yeyote maarufu na mwenye pesa hii ni kutokana na mpenzi wake wa zamani kukataa kurudiana naye,”Tunajua kwa sasa una hasira sana na kila mtu baada ya mzazi mwenzio wa zamani kukataa kurudiana na wewe, kumbuka yule mtoto uliyezaa naye ni damu yako lakini hujali“.
Akizungumzia kuhusu muziki wake kwa sasa Mayweather amesema “hauna tena ngoma kali (Hit Song) kwenye radio kama tulivyokuzoea miaka ya nyuma, kwa sasa hauna hata uwezo wa kuuza ngoma zako kwenye soko ndio maana Interscope (Lebo ya Muziki) imekupiga chini. Umekuwa mtu wa chuki kwa kila rapper, mwanamichezo na hata wachekeshaji ambao wanaingiza mkwanja mrefu au kufanya vizuri kwa sasa,” .
Mayweather akizungumzia bifu ya 50 Cent na Ja Rule amesema “unajifanya unamzonga Ja Rule ili upate kwa kutokea ile hali wewe ndiye uliyeiba staili zote za kurap kutoka kwa Ja Rule, ukatuletea staili zako za Ugangster sasa uko wapi? unaishi kwenye apartment za kimasikini huko New Jersey. nadhani kazi yako kwa sasa ni bora uwe blogger unaweza ukaingiza fedha ila sio muziki tena. Heti unanichukia badala ya kujilaumu Kanye West kakumaliza kwenye muziki,“.
Mwanamichezo huyo tajiri zaidi duniani amemuonya pia 50 Cent kuwa asije tena kumuomba au kumuazima fedha huku akimsema kuwa amekuwa mtu wa kupenda vitu vya kiki na umbea kuliko hata kazi yake ya muziki.
Mapema mwezi uliopita 50 Cent alimuita Floyd Mayweather ‘Mtu mjinga zaidi duniani’ baada ya mwanamasumbwi huyo kununua saa yenye gharama kubwa zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.