ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 7, 2018

BRAZIL, URUGUAY ZAWAACHIA UBINGWA WA DUNIA TIMU ZA ULAYA.Baada ya Brazil kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ubelgiji kwenye mechi ya robo fainali uliopigwa usiku wa jana, sasa imekuwa rasmi bingwa wa mashindano atatokea Bara la Ulaya.

Brazil na Uruguay ambazo zote zinatokea Amerika ya Kusini ndio timu pekee zilizokuwa zimebaki kwenye mashindano ambazo hazitokei bara la Ulaya lakini zote zimeondolewa ikianza Uruguay kwa kuchapwa bao 2-0 na Ufaransa na sasa imefuata Brazil.

Ubelgiji imeweka rekodi ya kucheza mechi 25 bila kufungwa huku pia ikiwa ndio timu yenye wachezaji wengi waliofunga mabao kwenye fainali hizi wakifika 9 ikizidiwa na Ufaransa mwaka 1982 na Italia mwaka 2006 ambapo walifunga wachezaji 10 tofauti.

Kwa upande wa Brazil, wao wameendelea na rekodi mbaya dhidi ya timu za Ulaya ambapo imeondolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia za hivi karibuni mara 4 na timu kutoka bara la Ulaya.

Iliondolewa na Ufaransa mwaka 2006, Uholanzi mwaka 2010, Ujerumani mwaka 2014 na Ubelgiji mwaka 2018. Ubelgiji sasa itacheza na Ufaransa kwenye nusu fainali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.