Na Zephania
Mandia/GSengoTV,
WADAU wa haki za binadamu wakiwamo waandishi wa
habari, wamesema jitihada za haraka zinatakiwa kuchukuliwa na vyombo vya dola
nchini, kukomesha mateso yanayowaandama wafanyakazi wa majumbani.
Kulingana na hayo, watoto wadogo wanaotumikishwa
kazi za majumbani kinyume cha sheria ni vema wakaokolewa, huku rushwa ikitajwa
kuwa ni tatizo linalokwamisha upatikanaji wa haki zao.
Hayo yamejiri katika semina inayoendelea jijini
Mwanza, iliyoandaliwa na Shirika la Kutetea Haki za Watoto na Wafanyakazi
Majumbani nchini (TDWC).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.