ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 21, 2018

TCRA YAKABIDHI VIFAA VYA HABARI KWA RC MONGELLA


NA. ZEPHANIA MANDIA/G.SENGO TV.

MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongella amekabidhiwa vifaa vya mawasiliano kwaajili ya kuboresha kitengo cha habari kwa ofisi ya mkoa. 

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Tanzania Injinia James Kilaba (kulia) amekabidhi vifaa hivyo ikiwa ni katika kutimiza adhama ya kuchochea shughuli za maendeleo ya mkoa na upashaji wa habari, elimu na taarifa wananchi wa Mwanza.

Aidha Mongella amewashukuru TCRA kwa kutambua changamoto iliyokuwa ikiikabili ofisi yake, akiahidi kuvitunza vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni ishirini.
Tayari Mongella ameshatenga chumba maalum kwaajili ya shughuli za  habari ili kutatua changamoto iliyokuwa ikiwakabili baadhi ya waandishi.
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.