ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 22, 2018

MUUGUZI WA KITUO CHA AFYA AWA MSHINDI WA KWANZA WA GARI KUTOKA VODACOM M-PESA



 GSENGOtV
Wateja Vodacom nchini wameanza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha na gari kupitia kampeni ya miaka 10 ya M-Pesa ambapo hii leo Jijini Mwanza Bi. Pasquiner Karol Ignas amekabidhiwa gari aina ya Renault Kwid yenye thamani ya shilingi Milioni 25.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia), akimkabidhi funguo, kadi na plate namba ya gari  wa mshindi wa nambari ya gari alilojishindia kupitia huduma ya M-Pesa. Bi. Pasquiner Korol Igans ni Muuguzi wa Kituo cha Afya Nyankumbu mkoani Geita.
Hafla ya kukabidhi zawadi hizo imeambatana na sherehe za miaka 10 tangu kuanzishwa huduma ya M-Pesa, iliyofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella.

Gari alilojishindia muuguzi huyo kupitia huduma ya M-Pesa. 
Rosalynn Mworia 
 Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rosalynn Mworia ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Vodacom Tanzania amesema huduma ya M-Pesa ilianza nchini mwaka 2008 na hadi sasa ina watumiaji zaidi ya Milioni nane huku ikichangia asilimia 37 ya pato la taifa.


Mhe.John Mongella
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella ameipongeza kampuni ya Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa kwa kuchangia ukuaji wa pato la taifa huku ikirahishisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo kufanya malipo ya umeme na maji.

Mshindi wa zawadi ya gari hilo, Pasquiner Karol Ignas ambaye Muuguzi wa Afya katika Kituo cha Afya Nyankumbu mkoani Geita, ameshindwa kuzuia hisia zake kwa furaha na kububujikwa na machozi, amewasihi watanzania kutumia huduma za Vodacom ikiwemo M-Pesa ambapo wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kama alivyoshinda.
Wakala Vedastus Lufano amejishindia shilingi Milioni moja kupitia huduma ya M-Pesa.
Wakala Mkurugenzi wa Kaliuwa Investiment Bi. Mwanabure akipokea cheti cha ufaniki kwa kufanya vyema kupitia huduma ya M-Pesa
Wakala akipokea cheti cha ufaniki kwa kufanya vyema kupitia huduma ya M-Pesa.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wadau mbalimbali mkoani Mwanza, wakifuatilia yale yaliyokuwa yakiendelea ndani ya hafla hiyo.
Wadau mbalimbali mkoani Mwanza, na zawadi zao mezani katika hafla hiyo.
Mc Magoma shughulini.
Wadau mbalimbali mkoani Mwanza, wakifuatilia yale yaliyokuwa yakiendelea ndani ya hafla hiyo.
Deejay K-Flip kutoka Jembe Fm ndiye muhusika katika muziki ndani ya hafla hii adhimu ya Vodacom.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.