ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 24, 2018

MAKONDA ATIMIZA AHADI YAKE KWA POLISI, AKABIDHI TANI 60 ZA SARUJI DAR.

NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

HATIMAYE Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo Juni 24/ 2018 ametimiza ahadi yake kwa Jeshi la Polisi aliyoitoa hivi karibuni kwa kuwakabidhi shehena ya Mifuko 1,200 ya Saruji sawa na Tani 60 yenye thamani ya shilingi Milioni 14 kwa Askari Bora 12 waliochaguliwa na Jeshi la Polisi kutokana na utendaji kazi mzuri.

Makonda amesema lengo la kutoa zawadi hiyo ni kujenga morali ya kazi kwa askari wanaojitoa kwa hali na Mali kulinda usalama wa Raia na Mali zao jambo linalopelekea Dar es salaam kuwa Shwari.


Mifuko hiyo ya Saruji imetolewa na kampuni ya Nabis Cooperate Ltd iliyounga mkono jitiada za Makonda katika kugusa maisha ya Wananchi katika masuala mbalimbali.

Aidha Makonda amesema pamoja na kuendelea kuliboresha Jeshi la Polisi Kama taasisi kwa kuwapatia vitendea kazi  Kama Magari, Pikipiki, Baiskeli na Computer pia ameona ni vyema kugusa maisha ya askari mmojammoja kwa kuhakikisha wanakuwa na makazi zao na familia  ili familia ijivunie kazi anayoifanya Baba au Mama.


Hadi sasa Makonda amewezesha zaidi ya askari Polisi 800 kupata mikopo ya viwanja vya bei nafuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabis Cooperate Ltd Eng. Thomas Wiso amesema kuwa wameamua kutoa saruji hiyo kuunga mkono jitiada za Makonda kujali wananchi wake na kuhakikisha hali ya Ulinzi na usalama inakuwa Shwari.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.