Vyumba 14 vya ghorofa moja katika Chuo cha Ushauri Nasaha na Uchungaji kilichopo Bugando jijini Mwanza, ambacho kinamilikiwa na kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mwanza vimeteketea kwa moto kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na hitilafu ya umeme.
Walioshuhudia tukio hilo, wamedai chanzo cha vyumba hivyo kuteketea kwa moto huo ni baada ya kukatika mara kwa mara kwa umeme kulikoanza majira ya saa 10 usiku. Wakati moto huo unatokea kwenye jengo hilo lenye jumla ya vyumba 28, vikiwemo vyumba vya madarasa, mabweni pamoja na maktaba hapakuwa na mwanafunzi yeyote.
Afisa wa Jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Nyamagana Inspekta Revocatus Magembe amesema kilichosababisha wao kuchelewa kuzima moto huo na kusababisha vifaa mbalimbali kuteketea ni kutokana na wahusika kushindwa kutoa taarifa mapema ya tukio hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.