ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 24, 2018

VIDEO;- SHUHUDIA MZIGO WA KWANZA KUSAFIRISHWA KWA TRENI TOKA MWANZA KWENDA UGANDA KWA NJIA YA MAJI NA MV UMOJA.NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
WAKAZI wa jiji la Mwanza hii leo wameshuhudia mzigo wa kwanza kusafirishwa kwa treni ya TRC kwenda Uganda baada ya zaidi ya miaka 10 ya kusitishwa kwa huduma za bandari kutokana na ubovu na uchakavu wa miundombinu ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafirishaji (meli) katika ziwa Victoria.

Mzigo huo umewasili leo jijini Mwanza na umefaulishwa kwa kuingia kwenye Meli ya Mv.Umoja tayari kwenda Bandari ya Port Bell nchini Uganda.

Hafla fupi ya Uzinduzi wa usafirishaji wa mabehewa ya mizigo kwa njia ya meli kupitia Ziwa Victoria kutoka Bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi Bandari ya Portbell (Uganda) imefanyika ikiwa ni hatua ya Kutekeleza ahadi iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya 5 ya Rais JPM ya kufufua miundombinu hiyo muhimu ya kiuchumi ili kuleta tija kwa wananchi na wafanyabiashara wa nchi zote mbili kwa kusafirisha mizigo kwa haraka na kwa gharama nafuu. 

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo amewahimiza wafanyabiashara ndani na nje ya nchi kutumia vyema fursa ya usafirishaji mizigo kupitia Ushoroba wa Kati (Central Corridor) unayohusisha njia ya reli na bandari.


Kwa muktadha huo sasa, ni ishara kwamba mizigo kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam itaweza kusafirishwa kwa njia ya reli hadi bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) na baadaye hadi bandari ya Portbell (Uganda) kupitia Ziwa Victoria ambapo meli ya MV.Umoja (yenye uwezo wa kubeba mabehewa 19) inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) itakuwa miongoni mwa meli zitakazosafirisha mizigo hiyo.


Wadau sehemu ya Meza kuu.
Mizigo huooooo.....
Meli ya Mv.Umoja ikijiweka tayari kwaajii ya kutia nanga na kupakia mzigo. 
Kamati.
Wadau sekta malimbali wakiwamo wafanyakazi wa TRL wafanyabiashara wakifuatilia hafla hiyo
Wadau sekta malimbali wakiwamo wafanyakazi wa TRL wafanyabiashara wakifuatilia hafla hiyo
Wadau sekta malimbali wakiwamo wafanyakazi wa TRL wafanyabiashara wakifuatilia hafla hiyo
Kamati ya ulinzi na usalama ndani ya tukio.
Sehemu ya wafanyabiashara mbalimbali wakifuatilia hafla hiyo
Mizigo kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam itaweza kusafirishwa kwa njia ya reli hadi bandari ya Mwanza Kusini na baadaye bandari ya Portbell kupitia Ziwa Victoria
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella na Mfanyabiashara Mr. Christopher Gachuma na meza kuu wakisherehekea sanaa na utamaduni wa ngoma ya Bujora.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.