Licha ya kuondosha makato ya viuwadudu, Soko la ushindani na mahitaji ya soko la dunia limeipelekea Serikali ya Tanzania kushusha bei ya pamba hadi shilingi 1,100/= kutoka 1,200/= bei ya zamani.
Waziri wa Kilimo, Dk
Charles Tizeba akipima moja ya mzigo wa pamba ya wakulima waliojitokeza wakati
wa hafla ya uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa zao hilo katika kijiji cha Bukama
wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Waziri wa Kilimo, Dk
Charles Tizeba akikata utepe kuzindua msimu wa ununuzi wa pamba wakati wa hafla
iliyofanyika kijiji cha Bukama wilaya ya Igunga mkoani Tabora Mei Mosi.
Waziri wa Kilimo, Dk
Charles Tizeba akifanya malipo kudhihirisha kuwa msimu huu malipo ni papo hapo iwe kwa fedha taslimu au kwa njia ya miamala ya fedha kupitia mitandao na njia za kibenki.
Kuhusu mikakati ya msimu ujao wa Kilimo, Dk Tizeba alisema Serikali itasambaza bure mbegu na viuatilifu na kuimarisha huduma ya ugani kwa wakulima ili kuongeza tija.
Aidha serikali imeapa kuwashughulikia wezi katika mizani za pamba ya wakulima na utaratibu wa kuweka mahakama zinazo tembea uko pale pale.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri ameapa kula sahani moja na viongozi waliochomoza tena kwenye uongozi wa vyama vya ushirika kwa kutumia rushwa ili wapate kutafuna haki za wakulima.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.