ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 1, 2018

JPM AAHIDI KUONGEZA MISHAHARA KABLA HAJAONDOKA MADARAKANI.

Iringa. Rais John Magufuli ameahidi kuwaongezea wafanyakazi mishahara kabla hajamaliza kipindi chake cha urais.

Rais Magufuli amesema hayo leo Mei Mosi katika Sikukuu ya Wafanyakazi iliyoadhimishwa kitaifa, Iringa.

Akizungumza katika Uwanja wa Samora zilimofanyika sherehe hizo, Rais Magufuli amesema kutokana na changamoto za kimaendeleo  zinazotakiwa kutatuliwa kwa sasa lakini Serikali itahakikisha inampa mfanyakazi maisha mazuri na nafuu kwa kudhibiti mfumuko wa bei ya bidhaa nchini.

"Natamani mwaka huu kupandisha mishahara kwa wafanyakazi lakini kutokana na changamoto zilizopo za kuajiri wafanyakazi 52,000 nitawalipa nini? nikisema natamka kuongeza mishahara, nitazipata wapi?”amesema Magufuli.

Rais Magufuli amesema iwapo wanataka waongezewe mishahara labda vyama vya wafanyakazi viuze miradi yao ili wajiongezee mishahara. Lakini hilo halitowezekana.

Amesema juhudi za Serikali kwa hivi sasa zimeelekezwa zaidi katika kuunda na kuboresha miundombinu ya miradi mbalimbali nchini ambayo muda mchache ujao ikikamilika na kuanza kuzalisha faida itaipa kiburi Serikali yake kuwa na uwezo wa kupandisha mishahara tena kwa viwango vizuri vyenye maana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.