ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 15, 2018

TUMEIBIWA TENA.


ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI: Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza bandarini katika eneo ambalo kuna matanki ya kuhifadhia mafuta ya kupikia, ambapo amesema hakuna tatizo lolote la mafuta na kwamba baada ya taratibu kukamilika, mafuta hayo yaliyokuwa yamekwama yataingizwa sokoni. Katika ziara hiyo Rais Magufuli amekuta aina mbili za mafuta (mafuta ghafi na mafuta safi) akisema kuwa amebaini udanganyifu katika utozaji wa kodi ambapo amekuta mafuta ghafi na mafuta safi yote yakitaka kutozwa kwa kiwango kimoja cha kodi cha mafuta ghafi. Pia amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara kufanya mchakato wa kupandisha tozo kwa mafuta ghafi yanayoagizwa kutoka nje ili kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya ndani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.