CHANZO/PARStODAY
Rais Donald Trump wa Marekani sambamba na kusema kuwa, ataweka wazi siku tatu zijazo nukta atakazozijadili pamoja na Kiongozi wa Korea Kaskazini, amesema kuwa, ni suala linalowezekana kuvunja ajenda ya mkutano huo.
Trump ameyasema hayo huku Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akiwa amefanya safari mjini Pyongyang na kukutana na Kim Jong-un. Akizungumza na waandishi wa habari waliomuuliza iwapo anaweza kuvunja kikao tarajiwa na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, Trump hakukadhibisha suala hilo. Amesema kuwa, pande zote mbili yaani (Washington na Pyongyang) zinataka kufikia makubaliano.
Serikali ya Korea Kaskazini imeionya Marekani kwamba sambamba na kukaribia kikao cha viongozi wakuu wa nchi hizo, Washington inatakiwa ijiepushe na uharibifu wowote wa anga ya mazungumzo hayo tarajiwa. Taarifa iliyotolewa na chama tawala nchini Korea Kaskazini imeashiria matamshi ya kila mara ya kupenda kujitanua yanayotolewa na viongozi wa Marekani hususan yanayosisitizia kuwekewa zaidi mashinikizo serikali ya Pyongyang. Kuhusiana na suala hilo chama hicho tawala nchini Korea Kaskazini kimesema kuwa ni muhimu sana kwa Marekani kujiepusha na anga ambayo inaweza kudhoofisha kufanyika mazungumzo tarajiwa kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong-un.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.