NA ZEPHANIA MANDIA/G.SENGO TV.
Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani,Wananchi wa mkoa wa Mwanza wameiomba serikali kufanya jitihada za haraka juu ya upatikanaji wa mafuta ya kula pamoja na sukuri ili kuepusha usumbufu wakati wa mfungo.
Wananchi hao wamesema kutokana na uhaba huo kumekuwepo na kupanda kwa bei mara kwa mara ya mafuta na sukari hivyo wananchi hao kushindwa kumudu kununua bidhaa hizo ambazo ni muhimu katika maisha ya kila siku.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELLA amefanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya maghala ili kuona kama kuna hali ya wafanya biashara kuhujumu zoezi la upatikanaji wa bidhaa hizo.
Akiwa katika maghala hayo MONGELA amebaini uwepo wa sukuri ya kutosha mkoa mzima pamoja na mikoa jirani huku ghala moja pekee likiwa na idadi ndogo ya maboksi ya mafuta.V.H. SHAH ni msambazaji wa bidhaa mablimbali ikiwemo sukari na mafuta ambapo ameeleza upatikanaji wa sukuri ya kutosha,huku akiwa hana uhakika wa upatikanaji wa mafuta licha ya kuhaidiwa.
Bei ya mafuta kwa lita mota kwa mkoa wa mwanza ni takribani shulingi elfu nne huku sukuri kilo moja ni kati ya shilingi elfu 2500 hadi elfu tatu,ambapo Momngela ametoa rai kwa wafanya biashara kutopandisha bei ya bidhaa hizo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.