Wanafunzi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maandamano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani 2018. Maandamano ya wanafunzi yalianzia eneo la Mission na kupokelewa katika uwanja wa Furahisha. Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Youth With New Hope in Life Organization (TAYONEHO), Dr.Imani Tinda akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Mgeni rasmi, Muuguzi Mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoani Mwanza. Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani 2018 yamefanyika kitaifa mkoani Dodoma, kama ilivyokuwa mwaka jana wakati yanaanza kuadhimishwa hapa nchini. Meneja wa shirika la Plan International mkoani Mwanza, Baraka Mgohamwende akiwasilisha salamu zake kwenye maadhimisho hayo. Upendo Abisai ambaye ni mwakilishi wa mradi wa Youth For Change unaotekelezwa na shirika la Plan International, akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo. Elizabeth Mbokela (katikati), ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyegezi akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wa kike mkoani Mwanza.
Pia shirika la Plan International limetumia maadhimisho hayo kutoa pedi kwa wanafunzi wa kike ili kuwasaidia kujisitiri wakati wa hedhi. Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani, ngazi ya mkoa. Wanafunzi kutoka shule za msingi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha. Wanafunzi wakionyesha igizo namna ukosefu wa elimu kuhusu hedhi unavyoweza kuwanyima mabinti uhuru wa kujiamini na kushindwa kuhudhuria masomo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la TAYONEHO FDr.Imani Tinda, Muuguzi mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan pamoja na Meneja Mradi (Boresha Elimu) kutoka shirika la TAYONEHO James Edward wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo. Tazama video hapa chini.
ISOME PIA HABARI HII Mwanza kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani 2018
Tanzania leo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani ambapo kwa mkoa wa Mwanza maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Furahisha.
Akisoma risala ya wanafunzi wa kike mkoani Mwanza, Elizabeth Mbokela ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyegezi amesema ni vyema serikali ikatenga bajeti kwa ajili ya kutoa bure taulo (pedi) kwa wanafunzi wa kike hatua itakayowasaidia kuondokana na changamoto ya kukosa masomo kutokana na hedhi.
Dr.Imani Tinda ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la TAYONEHO lililoratibu maadhimisho hayo kwa kushirikiana na Plan Internationa, amesema wanafunzi wa kike wamekuwa wakipoteza vipindi vya masomo kutokana na suala la hedhi ambapo kawaida mwanafunzi anapaswa kuhudhuria darasani siku 194 sawa na vipindi 1,740 lakini kutokana na hedhi wanafunzi wa kike huudhuria siku 84 sawa na vipindi 756.
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Muuguzi Mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan ametoa rai kwa kamati za shule kuhakikisha zinashiriki ipasavyo kuboresha mazingira ya wanafunzi wa kike hususani kutenga chumba maalumu kwa ajili ya kujisitiri wakati wa hedhi.
Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani hufanyika kila mwaka Mei 28 ambapo mwaka huu ni mara ya pili Tanzania kuadhimisha maadhimisho hayo tangu kuasisiwa na Umoja wa Mataifa UN mwaka 2014.
Mwaka huu kitaifa kaulimbiu ni “kila siku inaweza kuwa siku siku nzuri hata kama ni siku ya hedhi” huku kimataifa ikiwa ni “hakuna tena mipaka” kauli zote zikilenga kuhamasisha jamii kutakuwa kwamba hedhi ni suala la kawaida lisilopaswa kuleta vikwazo vya aina yoyote kwa wasichana na wanawake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.