ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 29, 2018

LIVE - WABUNGE WAKIAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA BUYUNGU, MWL KASUKU BILAGOGSENGOtV

Shughuli hii ya kutoa heshima za mwili inafanyika muda huu katika viwanja vya Bunge, Dodoma. Mara baada ya shughuli hii, mwili huo utasafirishwa kwenda Kigoma kwa maziko. Marehemu Kasuku Bilago alifariki dunia Jumamosi Mei 26, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

WABUNGE WAMUAGA ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA BUYUNGU

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya MakaziMhe Dkt Angeline Mabula jana katika viwanja vya Bunge wakiongozwa na Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe Dkt Tulia Ackson jana Mei 29, 2018 kwa pamoja wameshiriki ibada ya kumuombea na kumuaga aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu marehemu Mwalimu Kasuku Samson Bilago aliyefariki Mei 27, 2018 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Marehemu Mwalimu Kasuku Samson Bilago anatarajiwa kuzikwa   kesho Alhamisi Mei 31, 2018


'Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe'

.
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.