ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 29, 2018

BUIBUI-MTU APEWA URAIA UFARANSA KWA KUMUOKOA MTOTO ASIANGUKE GHOROFANI

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametoa amri ya kupewa uraia Mamoudou Gassama mhamiaji kutoka Mali ambaye ameonesha ushujaa mkubwa wa kukwea kwa umahiri wa kipekee dari za nyumba za jengo kubwa la ghorofa na kumuokoa mtoto aliyekuwa anakaribia kuanguka.
Mwanamme huyo kutoka Mali anaendelea kupongezwa kote nchini Ufaransa kwa ushujaa wake huo na ameshapewa uraia kwa amri ya Rais Emmanuel Macron.

Macron ametangaza kuwa, Mamoudou Gassama mhamiaji anayeishi nchini Ufaransa kinyume cha sheria, kuanzia sasa atakuwa raia wa kawaida wa Ufaransa na atajiunga na kikosi cha Zima Moto.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akizungumza na Mamoudou Gassama

Kundi kubwa la watu waliokuwa wamekusanyika kusubiri kuona hatima ya mtoto huyo aliyekuwa ananing'inia ghorofani na kuweko uwezekano wa kuanguka wakati wowote, walichukua filamu za video zinazomuonesha Gassama akikwea ghorofa za jingo hilo kama buibui hadi alipomfikia mtoto huyo na kumuokoa na kifo.

Majirani waliokuwa wanajaribu kumfikia mtoto huyo walishindwa kumuokoa. Baada wa Gassama kumfikia mtoto huyo na kumuokoa, kundi la watu lililokuwa limekusanyika chini ya jingo hilo lilipiga mayowe makubwa ya furaha na kumpongeza 'buibui-mtu' huyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.