Wakizungumza na waandishi wa habari jijini hapa ndani ya ofisi za msikiti wa Ijumaa Kati, waumini hao wamesema kuwa wamepata nguvu ya kwenda mbele na kudai haki yao kufuatia agizo la Rais Dkt John Magufuli alilolitoa mnamo mwaka 2016 wakati akihutubia Baraza la Eid la kuwataka wale wote waliopora mali za waumini wa dini ya kiislamu kuzirejesha.
Moja ya hoja walizosimamia wakati wa uwasilishaji watamko hilo ni pamoja na waumini hao kudai kuwa baadhi ya wadau walioingia kwenye madaraka ya shule hiyo wamewaondoa viongozi wengine kinyemela na kuugeuza mradi kuwa wa familia huku wakiwatuhumu kutumia mwanya huo kufanya biashara kwa kutumia vibaya misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini na kujinufaisha.
Madai mengine ni pamoja na waumini hao wakidai kupewa vitisho pindi wanapo ibua suala la kujua faida, mapato na matumizi ya shule hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.