Dar es Salaam, Aprili 16, 2018. Kampuni ya Taxify inayokuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika katika utoaji wa huduma zake za usafiri kwa njia ya mtandao, imetambulisha huduma nyingine mpya inayopatikana kwenye 'App' yake itakayofahamika kama 'Taxify XL'.
Kipengele hicho kipya kwenye app ya Taxify kimelenga kurahisisha usafiri katika maeneo mengi zaidi jijini Dar es Salaam.
Taxify XL (kubwa zaidi) ni kipengele ambacho kinawahusu wasafiri wanaokuwa kwenye kundi la takribani watu saba (7). Dhumuni la Taxify kuleta aina ya magari yanayochukua watu wengi, imetokana na matakwa ya wateja ambao wengi wa huduma ya usafiri wa magari makubwa.
"Kipengele cha XL ni mojawapo ya huduma mahususi kwa wale wanaosafiri katika makundi makubwa. Tayari tunatoa huduma kuanzia kundi la watu wanne kwa huduma ya Taxi za kawaida, Watu watatu katika kipengele cha bajaji. Na sasa huduma hii mpya ya XL itawapa watu fursa ya kusafiri hadi watu 7, " alisema Shivachi Muleji, ambaye ni Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki.
Kwa upande wake, Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini, Remmy Eseka alisema Taxify ni kampuni ya kwanza ya masuala ya usafiri ambayo inatoa huduma hiyo hapa jijini Dar es salaam.
Aliongeza kuwa ni huduma kwa kila mtu lakini hasa inakusudia kundi fulani la watu wanaosafiri kuelekea sehemu fulani kwa pamoja.
"Magari kama Toyota Alphard, Toyota Noah, Toyota Wish, Probox ni miongoni mwa magari ambayo wateja wetu watarajie kuyatumia kwenye huduma hii ya Taxify XL," alisema Eseka.
Eseka pia aliongeza kwamba madereva ya magari ya jumuiya ya XL, watatakiwa kupitia mafunzo kama ilivyo kwa madereva wanaotoa huduma zingine za Taxify.
Pia wanatakiwa kuwa na kadi za usajili wa magari, stika halali za bima pamoja na leseni za udereva.
Katika uzinduzi wa huduma ya Taxify XL kampuni hiyo imetoa punguzo la asilimia 20 kwenye usafiri huo. Gharama ya kuanza safari ikiwa ni Sh1,000, Sh 140 kwa dakika, Sh500 kwa kilometa, na Sh3,000 kama nauli ya kiwango cha chini. Taxify itawapa madereva malipo ya ziada kwa kila huduma kufidia punguzo hilo.
Taxify inachukua kamisheni ya asilimia 15 pekee kutoka kwa madereva wake, ambayo ni karibu nusu ya kiwango kinachochukuliwa na kampuni zingine zinazotoa huduma kama hiyo.
Hii inaiwezesha Taxify kutoa bei nafuu kwa wateja wake, huku ikitoa malipo mazuri kwa madereva hao.
Kwa jiji la Dar es Salaam, Taxify sasa inatoa huduma kwenye makundi matatu ambayo ni pamoja na Taxi:- (Gari za abiria wanne), Bajaji (iliyozinduliwa hivi karibuni) na sasa XL, ikiwa ni sehemu ya kampuni kuendeleza ubunifu na kuwa mbele katika ushindani.
-MWISHO-
Kuhusu Taxify
Taxify ni mojawapo ya kampuni shirikishi za usafiri zinazowaunganisha mamilioni ya madereva na wateja karibu ulimwenguni kote na kufanya huduma ya usafiri kuwa rahisi zaidi, haraka na kuaminika zaidi. Ufanisi na teknolojia ya Taxify imesaidia kuleta mabadiliko kwenye biashara ambayo inawanufaisha faida madereva ambao wanapata malipo ya kamisheni pamoja na abiria ambao wanalipia huduma kwa bei nafuu zaidi.
Taxify ilianzishwa na Markus Villig na ilizinduliwa mwaka 2013. Ni mojawapo ya kampuni inayokuwa kwa kasi miongoni mwa zinazoendesha huduma shirikishi ya usafiri hususani Ulaya na Afrika.
Nchini Tanzania, Taxify inafanya kazi jijini Dar es Salaam. Tangu mwaka 2017, Taxify inahusika katika ushirikiano wa kimkakati na Didi Chuxing, inayoongoza kwa utoaji wa huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao wa simu.
Taxify ina wateja zaidi ya milioni 5 katika nchi zaidi ya 20 duniani kote.www.taxify.eu
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.