Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa wito wa kurejeshwa amani katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwemo Syria na Yemen.
Akihutubia leo kwa mnasaba wa Sikukuu ya Pasaka, Papa Francis ametoa wito wa kuhitimishwa vita huko Syria, kurahisishwa kazi ya kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia na kuandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya kurejea makwao wakimbizi.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesisitiza katika ujumbe wake wa leo kwamba: "Kuna haja na kurejeshwa amani katika maeneo yote duniani hususan Syria nchi ambayo imetaabika kwa muda mrefu". Hali inayowakabili wananchi wa Syria kutokana na vita |
Papa Francis ameongeza kuwa mapigano na umwagaji damu unaoendelea sasa vimewaathiri raia wasio na ulinzi wa Yemen na eneo zima la Mashariki ya Kati.
Ujumbe wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani umetolewa katika hali ambayo Marekani na waitifaki wake yaani baadhi ya nchi za Magharibi na za Kiarabu zinatambulika kuwa chanzo kikuu cha machafuko katika eneo la Mashariki ya Kati hususan huko Syria. Utawala wa Aal Saud unaouungwa mkono na tawala za Magharibi tangu miaka mitatu iliyopita ulianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen na kuizingira kwa pande zote nchi hiyo maskini ya Kiarabu. Uvamizi huo wa Saudia umesababisha vifo vya maelfu ya raia wa Yemen na kujeruhi mamilioni ya wengine. Miundo mbinu ya Yemen kama barabara, shule, hospitali, misikiti na ofisi za umma pia zimebomolewa katika vita hivyo vinavyoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.