ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 15, 2018

DSTV WAFUNGUA HIMAYA MPYA JIJI LA MIAMBA

Oparesheni Meneja wa Multichoice Tanzania, Baraka Ronard Shelukindo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Center ya Huduma za DSTV Mwanza.

Katika kuhakikisha kuwa wateja wa mkoani Mwanza wanaendelea kufurahia huduma za DStv, kampuni ya Multichoice Tanzania imefungua Center ya huduma kwa wateja wake.

Awali wateja wa mkoa wa Mwanza na wilaya zake walikuwa wakipata huduma kutoka duka dogo la mauzo lililokuwa nje kidogo ya mji likiwa finyu kwa ofisi zake na hata uhudumiaji wateja lakini sasa ujio wa Center hii mpya unawapa fursa wananchi kupata huduma kwa wakati na haraka zaidi kwani hata watoa huduma wameongezwa kulingana na vitengo.

 Baraka Ronard Shelukindo ni Oparesheni Meneja wa Multichoice Tanzania, anasema kuwa ufunguzi wa Center hiyo ya Huduma kwa wateja ni sehemu ya harakati ya kampuni hiyo kuongeza kasi ya maboresho ili kuondoa kadhia kwa wateja wa DSTV ambao wamekuwa wakiongezeka kila uchwao kutokana na ubora wa vifurushi wanavyotoa kwa walaji vinavyolenga kiu na mahitaji ya maudhui ya soko la sasa.
"Hivi karibuni mtashuhudia tukifungua vituo vingi hapa nchini, ambapo kwa jiji la Dar es salaam pekee kutokana na mahitaji na ukubwa wake tunataraji kuongeza vituo viwili ikiwa ni mpango wa kuzikabili changamoto mbalimbali tulizobaini" alisema Shelukindo.

Meneja wa Mauzo mkoa wa mwanza John Kasuku (kulia) akimkabidhi Bwana Leo Atanas Mayunga mkazi wa Igombe wilayani Ilemela, zawadi ya T-Shirt baada ya kuwa mteja wa kwanza  kuingia kwenye Kituo hicho kipya mara baada ya uzinduzi. Mteja huyu pia alipata nafasi ya kutoa maoni yake sanjari na changamoto ambazo angependa zifanyiwe kazi.
Kiofisi zaidi.
 KUHUSU MAUDHUI
“Wateja wetu walituomba tuongeze maudhui ya kitanzania kwenye king’amuzi chetu, tukawasikia, tukaweka chanel maalum kabisa ya Maisha Magic Bongo ambayo ina asilimia 100 ya maudhui ya Kitanzania; wakatuomba tupunguze bei ya vifurushi, tukafanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana, na leo tena kwa mara ya pili tumepunguza bei, wakatuomba tuongeze chanel kwenye vifurushi vya bei ndogo, tukafanya hivyo, tukaleta LaLiga na Ligi Kuu ya Uingereza hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”. 

ZAWADI
Ndani ya uzinduzi huo waandishi wa habari watatu wa jijini Mwanza kila mmoja amejinyakulia zawadi ya BURE ya Seti kamili ya king'amuzi cha DSTV kilicho ambatanishwa na dishi lake, vocha ya kutizama Bure DSTV mwezi mzima sanjari na huduma ya ufundi.
Meneja wa Mauzo mkoa wa Mwanza John Kasuku (kulia) akimkabidhi mwandishi wa habari toka Clouds Fm Bi. Sara, zawadi ya BURE ya Seti kamili ya king'amuzi cha DSTV kilicho ambatanishwa na dishi lake, vocha ya kutizama Bure DSTV mwezi mzima sanjari na huduma ya ufundi, baada ya kushinda kupitia bahati nasibu ya wazi kwa wandishi.
Meneja wa Mauzo mkoa wa Mwanza John Kasuku (kulia) akimkabidhi mwandishi wa habari toka IPP Media George Ramadhan, zawadi ya BURE ya Seti kamili ya king'amuzi cha DSTV kilicho ambatanishwa na dishi lake, vocha ya kutizama Bure DSTV mwezi mzima sanjari na huduma ya ufundi, baada ya kushinda kupitia bahati nasibu ya wazi kwa wandishi.
Meneja wa Mauzo mkoa wa Mwanza John Kasuku (kulia) akimkabidhi mwandishi wa habari toka Star Tv Soud Shahban, zawadi ya BURE ya Seti kamili ya king'amuzi cha DSTV kilicho ambatanishwa na dishi lake, vocha ya kutizama Bure DSTV mwezi mzima sanjari na huduma ya ufundi, baada ya kushinda kupitia bahati nasibu ya wazi kwa wandishi.
Jiografia ya tukio.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.