Mgeni rasmi Mhe. Mchembe akipokea taarifa ya Wanawake Gairo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Gairo, Agnes Mkandya.
Uongozi wote wa Wilaya ya Gairo, upande wa Chama na Serikali ukielekea kwenye kupanda miti kuashiria alama ya uhai mpya kwa wanawake waliokata tamaa.
Viongozi wakiwa fuatilia.
Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya akitoa salamu.
Mkurugenzi wa Halmashauri, Mhe. Rahel Nyangasi akitoa salamu.
Viongozi Wanawake wa Wilaya ya Gairo wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (wa pili toka kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Nyangasi (watatu kushoto) na Agnes Mkandya wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya siku ya Wanawake Duniani. Wilaya ya Gairo inaendeshwa na wanawake kwa asilimia zaidi ya 95 (tisini na tano).
Wanawake wakipima VVU wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani humo.
Akinababa nao walijitokeza kuomba msaada wa kisheria.
Na Mwandishi Wetu.
Wilaya ya Gairo imefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8 kupanda miti ili kuashiria uhai kwa wanawake waliokata tamaa.
Zoezi hilo liliongozwa na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe na wanasheria wanawake sita akiwemo Mwanasheria wa Manispaa Mvomerowaliweza kusikiliza kero za muda mrefu za wanawake.
Masuala yaliyoangaliwa katika maadhimisho hayo ni migogoro ya ardhi, mirathi, unyanyasaji kijinsia, ukeketaji na kesi za mimba za utotoni ambapo zaidi Wanawake zaidi ya 65 waliweza kuhudumiwa.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo wakati wakiendelea katika Uchumi wa Viwanda, "Tuimarishe usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake vijijini", ambapo ulipokelewa kwa shangwe na wanawake kijiji cha Kisitwi jambo lililomvutia Mkurugenzi Bi. Agnes Mkandya na kugawa miche ya korosho zaidi ya elfu 40, mbegu za pamba na kahawa.
Mhe. Mchembe alisisitiza wanawake kulima Kilimo cha Kibiashara ili kuinua kipato na uchumi wao waondokane na utegemezi.
Mkuu wa Wilaya huyo ameziomba Taasisi za kifedha NMB na CRDB kutoa mikopo kwa wanawake yenye riba nafuu, aidha kabla ya mkopo wanawake wapewe Elimu ya fedha, masoko, vifungashio, Sheria mbambali na ujasiriamali katika mapana yake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.