ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 24, 2018

MTOTO HUYU MLEMAVU KUSOMESHWA HADI NGAZI YA CHUO KIKUU


NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO TV
TAASISI YA KIMATAIFA YA JOSEPHAT TORNNER FOUNDATION (JTF) IMEAHIDI KUMSOMESHA KUANZIA DARASA LA KWANZA, HADI CHUO KIKUU, MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MACHO, SUNDI MASALU, KUANZIA SASA.

MKURUGENZI WA TAASISI HIYO INAYOHUSIKA NA USAIDIZI WA WATU WENYE ULEMAVU, JOSEPHAT TORNNER, AMEUHAKIKISHIA ULIMWENGU HAYO JANA, ALIPOZUNGUMZA MBELE YA WAZAZI NA VIONGOZI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA MALILI, WILAYA YA BUSEGA MKOANI SIMIYU, MUDA MFUPI KABLA YA KUKABIDHIWA MTOTO HUYO KWENDA KUMHUDUMIA KIELIMU.

KWA UPANDE WAO, BABA NA MAMA WA WA MTOTO SUNDI, GRESS MAYALA NA MASALU BONIPHACE, WAMEUSHUKURU UONGOZI WA TAASISI YA JTF KWA UAMUZI WA KUANZA KUMSOMESHA MTOTO WAO HUYO, HUKU WAKIOMBA WALEMAVU WENGINE WAPATE MISAADA KAMA HIYO.BAADA YA HAPO, TORNNER AKAKABIDHIWA MTOTO. SAFARI YA SUNDI YA KUVUKA MILIMA NA MABONDE IKAANZIA HAPA NYUMBANI KWAO, KUELEKEA KATIKA SHULE YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU YA BUHANGIJA, ILIYOPO MKOANI SHINYANGA.
ALIPOWAILI MKOANI SHINYANGA, SUNDI AKAPOKELEWA NA OFISA ELIMU TAALUMA WA SHULE ZA MSINGI, MANISPAA YA SHINYANGA, ESAU NYERIGA, PAMOJA NA UONGOZI WA SHULE. WAKAWA NA HAYA YA KUSEMA.
HAPA NI BUHANGIJA SHULENI KWA SUNDI. ANAANZA MAISHA MAPYA BAADA YA MIAKA TISA BILA KUIJUA ELIMU. KISHA SUNDI AKASEMA KWA LUGHA YA KISUKUMA YA BABA NA MAMA YAKE.

BAADA YA MTOTO HUYU KUKABIDHIWA TAYARI KWA KUANZA MASOMO YAKE YA DARASA LA KWANZA, KATIKA SHULE YA BUHANGIJA MKOANI SHINYANGA, TORNNER AKATOA USHAURI.

MTOTO SUNDI MASALU, MWENYE NDOTO YA KUWA NESI AU MWALIMU, AMEIBULIWA NA TAASISI YA JTF, KUPITIA KAMPENI YAKE YA PAZA SAUTI KUMLINDA MTOTO MWENYE ULEMAVU KIELIMU.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.