ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 22, 2018

COCA COLA YAJA NA PROMOSHENI YA 'MZUKA WA SOKA NA COKA'

 Maofisa wa kampuni ya Coca-Cola mkoani Mwanza, kutoka kushoto Meneja Mauzo Mkoa , Mnyamuhanga Gavana,Meneja Mauzo na Masoko Samuel Makenge na Meneja Mauzo Mwandamizi Deus Kadico, wakionyesha mfano wa chupa zenye vizibo vyenye zawadi ya promosheni ya ‘Mzuka wa Soka na CoKa’ iliyozunduliwa jijini humo.
Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya soda ya Cocacola tawi la Mwanza Samuel Makenge, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni.

* Lengo ni kuwezesha wapenzi wa soka kupata burudani ya Kombe la Dunia 2018

Wakati michuano ya Kombe la Dunia 2018, ambayo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya Coca-Cola inakaribia kuanza,kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Nyanza Bottlers leo imezindua promosheni itakayotoa fursa kwa wateja wake kujishindia luninga za kisasa, zitakazowezesha kufaidi uhondo wa michuano ya kombe la dunia wakiwa majumbani kwao.

Promosheni hii ambayo inajulikana kama ‘ Mzuka wa Soka na CoKa’ itawahusu watumiaji wa soda za Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparleta na Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kanda ya ziwa .

Mbali na zawadi za televisheni,watumiaji wa vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola, kupitia promoheni hii wataweza kujishindia zawadi nyinginezo mbalimbali ikiwemo ,fedha taslimu kati ya shilingi 5,000 mpaka shilingi 100,000/-kofia, t shirt,soda za bure na zawadi kubwa ya bodaboda.

Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya Nyanza Bottlers,Samwel Makenge ,amesema Coca-Cola ikiwa ni mdhamini mkuu wa mashindano ya Kombe la Dunia 2018,imekuja na promosheni ya kuleta shangwe za mashindano hayo katika mkoa wa Mwanza,utakaowawezesha wateja wake kufurahia mashindano haya ya soka makubwa duniani wakati huohuo wakiburudika na vinywaji vya Coca-Cola na kujishindia zawadi kemkem.

“Wakati michuano ya Kombe la Dunia inakaribia kuanza,tumeona tuje na promosheni hii ambayo itawezesha watumiaji wengi wa vinywaji vya kampuni yetu kujisindia luninga za kisasa aina ya SONY LED zenye kioo cha mbele bapa ili wapate uhondo wa mashindano hayo.Kinachotakiwa ni kunywa soda na kushinda zawadi”.Alisema Makenge.

Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Nyanza Bottler,Japhet Kisusi,alisema ili kujishindia zawadi anachotakiwa kufanya mtumiaji wa soda ni kuangalia ganda la chini ya kizibo baada ya kunywa soda linakuwa na picha ya zawadi aliyobahatika kujishindia. “Kwa upande wa zawadi ya pikipiki anachotakiwa kufanya mteja ni kuunganisha picha tatu vinavyokamilisha picha ya pikipiki kutokana na ganda atakalokuta ndani ya soda.kuna sehemu ya mbele,kati na nyuma.Zawadi zote kubwa zitachukuliwa kiwandani na ndogo kama kofia,T shirt na soda za bure zitatolewa na mawakala wa kampuni waliosambaa maeneo mbalimbali”.Alisisitiza.

Kwa upande wake,Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini,Sialouise Shayo,alisema promosheni hii inadhihirisha dhamira ya kampuni ya kuwawezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla kupata 'Mzuka wa Soka na Coka' katika msimu wa kombe la Dunia na kujisikia sehemu ni sehemu ya mashindano hayo.

Katika maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Dunia 2018,Coca-Cola imetangaza hivi karibuni kuwa msanii mmoja wa Tanzania atashirikiana na mwanamziki nguli wa kimataifa, Jason Derulo ,kutengeza wimbo maalumu wa mashindano hayo wenye vionjo vya Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.