Chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kilmewalisha hoja bungeni kikitaka kumsaili na kumuuzulu Rais Edgar Lungu wa nchi hiyo. Chama hicho kinamtuhumu Rais Lungu kuwa amekiuka katiba. Hayo yameripotiwa leo na ofisi ya Rais wa Zambia.
Hoja hiyo iliyowasilishwa na chama kikuu cha upinzani cha UPND imesainiwa na theluthi moja ya wawakilishi wa Bunge la Zambaia lenye jumla ya wabunge 166. Ili iweze kuidhinishwa, kwa ajili ya kumsaili na kumuuzulu Rais wa Zambia, hoja hiyo inapasa kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge.
Msemaji wa Rais wa Zambia, Amos Chanda amesema kuwa huu ni mwendelezo wa jitihada zilizofeli za chama kikuu cha upinzani (UPND) za kuwasilisha hoja mahakamani kupinga ushindi wa Rais Edgar Lungu.
Hoja hiyo inatarajiwa kujadiliwa wiki ijayo tarehe 28 mwezi huu. Hoja hiyo inaeleza kuwa, Rais Lungu alikiuka katiba kwa kutokabidhi madaraka kwa Spika wa Bunge la Taifa wakati mrengo wa upinzani ulipopinga mahakamani ushindi wake mwaka 2016. Rais Lungu alichuana vikali na hasimu wake kutoka chama cha UPND, Hakainde Hichelema.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.