ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 11, 2018

AZAM FC YAZAMISHA MISUMARI MIWILI KWA MBAO FC.


Azam FC imerejea tena kwa muda kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, baada ya kuifunga Mbao FC kwa mabao 2-1.

Ikiwa Uwanja wake wa nyumbani, Azam ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Idd Kipagwile akifunga dakika ya 63.

Baada ya bao hilo, ilichuka dakika saba pekee ambapo Bernard Arthur alifunga bao la pili katika dakika ya 72 ya mchezo.

Bao pekee la Mbao lilifungwa na James Msuva, dakika ya 90 na Emmanuel Mvuyekure.

Matokeo hayo yanifanya Azam kuwa juu ya Yanga kwenye msimamo wa ligi kwa muda, ikifikisha alama 44 dhidi ya Yanga yenye 43.

Yanga itarudi kwenye nafasi endapo itashinda mchezo wake wa kesho dhidi ya Stand United utakaopigwa Uwanja wa Taifa.


MATOKEO KWA MICHEZO MINGINE.
Ruvu Shooting imegoma kupapaswa nyumbani baada ya kwenda sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbeya City FC.

Singida United ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani, Namfua Stadium, imelazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Ndanda FC kutoka Mtwara.

Majimaji FC imezidi kujiweka kwenye mazingira magumu baada ya kupata suluhu ya 0-0 dhidi ya Lipuli FC yenye maskani yake mjini Iringa.

Nayo Mtibwa Sugar iliyosafiri kuelekea mjini Mbeya, imekubali kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons, mechi ikipigwa Uwanja wa Sokoine. Mabao ya Prisons yamefungwa na Kimenya katika dakika ya 45 na 49, huku la Mtibwa likifungwa na Mbonde dakika ya 32.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.