Katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda kwa mabao 4-0.
Bao la leo la Simba lilifungwa na Emmanuel Okwi, Simba ikiwa imekianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa.
Mechi hiyo ilikwenda mapumziko kwa sare ya bila bao huku Gendamarie wakipoteza nafasi moja ya kufunga na Simba wakipoteza tatu ikiwemo ya Okwi aliyekuwa nahodha katika mchezo wa leo.
Al Masry. |
Mafarao wa Misri, Al Masry licha ya kufungwa mabao 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia, Al Masry imefuzu na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya ushindi wao wa mabao 4-0 wakiwa nyumbani Misri na sasa hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho, wanakutana uso kwa uso na Simba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.