Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Joseph Iha akizungumza na wageni waalikwa na wanahabari waliofika katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.
Wateja walihudhuria uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayotolewa na benki ya Equity jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Joseph Iha (wa pili toka kushoto) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa. Pembeni ni wakurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo ikiongozwa na Simbeye.
Picha/Habari: Cathbert Kajuna -Kajunason/MMG.
Benki ya Equity imezindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ambapo wateja wao sasa watapata huduma mahali popote kupitia simu za mkononi, tablets na kompyuta za mezani na mpakato.
Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Eazzy Banking, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Joseph Iha amesema kuwa huduma hizo mpya zitatoa fursa kwa wateja kufanya miala mahali popote.
Huduma hizo watazipata kupitia Eazzy Banking kwa kufanya miamala kirahisi iwe usiku au mchana, wakiwa nyumbani, au ofisini na kubwa zaidi sasa watakuwa na nafasi ya kuokoa muda na gharama.
"Huduma za Eazzy Banking zitaambana na EazzyBanking App, app ya kimataifa ya masuala ya kifedha inayounganisha huduma za laini za simu na kuwawezesha wateja kutuma fedha na pia kufanya malipo kupitia simu zao popote walipo na wakati wowote.
"EazzyBanking ni rahisi kuianzisha na hutoa huduma za kipekee kama kutuma fedha kwenda akaunti za benki au mitandao ya simu, kuomba na kulipia mikopo , kulipia bili(ankara) na aina ya huduma za malipo," amesema Iha.
Amefafanua kwa wale wenye simu za kawaida, kuna suluhisho kwao ambalo linajukulikana kama Eazzy24/7. Huduma hiyo ambayo imeboreshwa inawezesha watumiaji kupata huduma zilezile kama za EazzyBanking App kwa kupigiga *150*07# kupitia simu zao.
Ameongeza ndani ya huduma hiyo kuna kipengele cha huduma ambacho mtandaoni unaweza kufanya manunuzi ya rejareja ambapo wateja wataendesha akaunti zao na hiyo inajulikana kama EazzyNet; huduma ya malipo mbalimbali inayoitwa EazzyPay ambayo huwezesha kufanya malipo ya bili kama ving'amuzi, Tanesco, Luku na Dawasco.
Pia amesema inawezesha kununua na kulipia bidhaa na huduma kupitia kwa wauzaji waliosajiliwa kama Supermarket na hoteli kwa pale unapoona bango au stika ya "EazzyPay inakubalika hapa".
"Huduma ya mkopo kwa njia ya simu inayoitwa EazzyLoan pamoja na uvumbuzi na usimamizi wa fedha kwa SMEs /wafanyabiashara wa kati na wateja wakubwa, kampuni kubwa au Wizara kwa kupata huduma kupitia EazzyBiz.
"Pia kuna EazzyKikundi ambayo hiyo inatoa nafasi ya kusaidia Saccos, Viccoba, vikundi vya kiuchumi na uwekezaji na utunzaji kumbukumbu za biashara,"amesema na kusisitiza kupitia EazzyBanking wateja watapata huduma za kibenki kirahisi , salama na bila stress, "amesema Iha.
Akifafanua zaidi amesema uzinduzi wa huduma hiyo ya kibunifu unaongozwa na huduma mama ya EazzyBanking App ambayo itaimarisha mbinu mkakati za kibenki katika kuwahudumia wateja kimtandao kutokana na mabadiliko ya mahitaji yao.
Amewahakikisha Watanzania kuwa benki hiyo ipo makini katika kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuomba wale ambao hawajajiunga na benki hiyo huu ndio wakati sahihi kwani mambo yote ya kibenki unayafanya bila Stress.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.