Mbali na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Kitambi ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha, Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert Msando.
Akizungumza mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano, moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa."
Kwa upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani.
Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho.
"Mwenyekiti wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie, kudumu Chama cha Mapinduzi," amesema Masha.
Kwa upande wake Mwigamba amesema hoja zote walizopigania Rais John Magufuli kwa sasa anazitekeleza. Kutokana na hali hiyo analazimika kumuunga mkono.
"Lakini ni bahati mbaya wapo wanaoamini upinzani ni kama, tumeamua kuwa moto, wanaposema huyo amenunuliwa, mie ndiyo naendelea kuwa moto.”
Yeye Msando amesema baada ya kutoka Chadema kwenda ACT amejitambulisha rasmi kujiunga na chama hicho.
Amesema anafarijika kuona chama hicho na haoni aibu kuwa karibu na CCM tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani kwani wanachama walihofia kuvaa mavazi ya chama hadharani kwa kuogopa kuzomewa.
"Kwa sasa chini ya uongozi wako, mtu anajivunia kuwa mwanachama wa CCM, tukaona juhudi zinazoendelea," amesema Msando.
YALIYOSEMWA LEO JUMANNE NOVEMBA 21, 2017 KWENYE KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC) TAIFA, IKULU
1. “Waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali ni 3004 na nafasi za wanaohitajika ni nafasi 201” – JPM
2. “Tulifanya magaeuzi makubwa ili kukirejesha chama kwa Wanachama na kurejesha imani ya CCM kwa Watu” – JPM
3. “Mageuzi haya yamekuwa miiba mikali kwa waliozoea kukichezea chama chetu” – JPM
4. “Kila siku Watu wanarejea CCM, ni ishara ya kupendwa vilivyo kwa CCM” – JPM
5. “CCM inahitaji viongozi wanaochukizwa na rushwa, uonevu, ubadhilifu. Wanaopenda kutimiza ahadi za TANU” – JPM
6. “Wajumbe msije na majina yenu mifukoni, mnaweza kurudi nayo yakiwa huko huko mifukoni” – JPM
7. “Nina imani na uchambuzi uliofanywa na Sekretariet. Kwa wale ambao hawataridhishwa na mgombea yeyote, nimekuja na mafaili ya wagombea wote nitamwonyesha” – JPM
8. “Hapa ni kwenu, bila ya nyinyi (Wajumbe) nisingefika hapa. Mna kila sababu ya kufanya kikao hapa" - JPM
9. “Katika siku za hivi karibuni tumeona mapinduzi ya kiutawala, kiitikadi, kiuchumi” – Dk. Mkumbo
10. “CCM ndio chama pekee kinachoonekana kina nguvu hapa nchini” – Dk. Mkumbo
11. “Nimekubali kurudi kwa dhati, ninaomba ridhaa nirudi mnipokee” – Lawrence Masha
12. “Nimerudi zizini nikiwa na mkia, nipo tayari kutumika” – Lawrence Masha
13. “Yale tuyotarajia Wapinzani tuyaone yakifanyika, yanafanyika katika utawala wako Rais Magufuli, tuna kila sababu ya kukuunga mkono” – Samson Mwigamba
14. “Kadri wanavyopiga kelele, ndivyo wewe unazidi kupanda mlima” – Samson Mwigamba
15. “CCM ni chama kinachoonyesha kuwajali watu, mimi kama kijana ninajivunia kuwa Mwanachama wa CCM” – Alberto Msando
16. “CCM kilihaidi kupambana na umaskini, kutengeneza ajira, kurudisha nidhamu na uwajibikaji. Tuna kila sababu ya kupongeza kwa haya mambo mazuri” – Alberto Msando
17. “Leo hii nasaliti ubinafsi, ukabila, umimi kwa kuamua kujiunga na CCM” – Patrobasi Katambi
18. “Upinzani wa leo unajadili mambo binafsi na matukio kuliko kujadili namna ya kulisaidia Taifa” – Patrobas Katambi
19. “Kijana ndani ya upinzani ni karai linalojenga ghorofa. Karai huonekana takataka baada ya ghorofa kukamilika” – Patrobasi Katambi
IMEANDALIWA NA;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM TAIFA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.