KUTOKA Nairobi nchini Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kuongoza Kenya kwa muhula wa pili wa miaka mitano na wa mwisho katika sherehe zilizofana na ameahidi katika hotuba yake kuondoa viza na kukutana na wanasiasa kwa masilahi ya Kenya.
"Naapa kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatii, nitahifadhi, nitalinda na kutetea Katiba ya Kenya kwa kuzingatia sheria, na nitazingatia sheria zote; na kwamba nitalinda na kusimamia kikamilifu utaifa, uadilifu na heshima ya watu wa Kenya,” alisema Kenyatta huku akiwa ameshika Biblia kwa mkono wa kulia alipokuwa akila kiapo cha kuingia ikulu.
Biblia hiyo, kwa mujibu wa Mkuu wa sherehe Duncan Okello, ni ileile iliyotumiwa na rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta aliyoishika wakati wa uhuru Desemba 12, mwaka 1963.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.