Waziri Mgalu aliyasema hayo tarehe 27 Novemba, 2017 kwenye ziara yake katika kituo cha kupoza umeme Kigamboni na katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kata za Kisiju na Mkamba zilizopo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja kutoka 6,000 hadi 12,000 na kuongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati itahakikisha vituo vingine vya kuboresha hali ya umeme ndani ya jiji la Dar es Salaam vinakamilika mapema Desemba 15, 2017 na kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara lililokuwa linajitokeza.
Aidha, alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha vituo vingine vilivyobaki vya Kurasini, Gongo la Mboto na Mbagala mapema ili wakazi wa jiji la Dar es Salaam waweze kuondokana na tatizo la ukosefu wa umeme.Katika hatua nyingine, Mgalu aliwataka wandarasi waliopewa kazi ya kujenga miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukamilisha miradi mapema na kuongeza kuwa Serikali haitamvumilia mkandarasi atakayezembea ukamilishwaji wa mradi wake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.