ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 9, 2017

RAIS WA TFF APONGEZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.

Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Oktoba 9, 2017 akiliapisha Baraza jipya la mawaziri, Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Wallace Karia, ametuma salamu za pongezi kwa mawaziri wote wapya.


Wallace Karia
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli alifanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri.

Taarifa ya Kurugenzi ya Ikulu iliyosainiwa na Gerson Msigwa, ilisema kwamba Mhe. Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alitangaza Baraza hilo  Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika mabadiliko Mhe. Rais Dk. Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21 na hapo ndipo akamteua tena Mhe. Dk. Harrison George Mwakyembe kuendelea kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Juliana Daniel Shonza kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kutokana na uteuzi huo, Rais wa TFF Karia amewapongeza Waziri Dk. Mwakyembe na Naibu wake, Shonza akisema: “Hongera sana viongozi wetu wapya wa wizara.”
Lakini pia nipongeze Baraza zima la Mawaziri. Tuna imani na viongozi wetu. Tunaomba mwenyezi Mungu awasaidie mawaziri wote katika kazi zao hasa ikizingatiwa kwamba tuna majukumu mazito katika mpira wa miguu katika mashindano ya kimataifa kwa mwaka ujao.

“Lakini kubwa zaidi, Tanzania tunaandaa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (AFCON-U17), sasa basi kwa kushirikiana na viongozi wetu wa wizara, tunaamini tutaweza. Tutafanikiwa,” amesema Rais Karia.

Mbali ya Mhe. Dkt. Mwakyembe na Juliana Shonza, wengine ambao waliteuliwa na kuapa leo Jumatatu ni George Mkuchika anayekuwa Waziri wa Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Mkuchika pia amewahi kuwa waziri mwenye dhamana ya michezo hapa nchini.
Wizara na Mawaziri wengine ni kama ifuatavyo.

Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi.
Waziri – Suleiman Jafo na Manaibu waziri – Josephat Kandege na Joseph George Kakunda.
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Waziri – January Makamba na Naibu Waziri, Kangi Lugola.
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Jenista Mhagama na Manaibu Stella Ikupa na Anthony Mavunde.
Wizara ya Kilimo.
Waziri ni Dk Charles Tizeba na Naibu wake Dk Mary Mwanjelwa.
Wizara wa Mifugo na Uvuvi.
Waziri ni Luhaga Mpina na Naibu wake ni Abdallah Ulega.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri ni Profesa Makame Mbarawa na Manaibu wake Atashasta Nditiye na Elias Kwandikwa.
Wizara ya Fedha na Mipango.
Waziri ni Dk Philip Mpango na Naibu waziri ni Ashantu Kijaji.
Wizara ya Nishati.
Waziri ni Dk Medard Kalemani na Naibu wake ni Subira Mgalu.
Wizara ya Madini.
Waziri ni Angellah Kairuki na Naibu wake Haruni Nyongo.
Waziri wa Katiba na Sheria.
Waziri ni Profesa Palamagamba Kabudi
Wizara wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri ni Dk Augustino Mahiga na Naibu Dk Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Waziri ni Dk Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waziri ni Mwigulu Nchemba na Naibu wake Hamad Masauni.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri ni William Lukuvi na Naibu ni Angelina Mabula.
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Waziri ni Dk Hamis Kigwangala na Naibu wake ni Ngailonga Hasonga.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri ni Charles Mwijage na Naibu wake ni Stella Manyanya.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Waziri ni Profesa Joyce Ndalichako na Naibu wake ni  Wiliam Ole Nasha.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Waziri ni Ummy Mwalimu na Naibu wake ni Dk Faustine Ndugulile.
Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Waziri  ni Isack Kamwele na Naibu wake ni Juma Aweso.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.