ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 9, 2017

MAKUMI YA WATU WA ROHINGYA WAFA AMJI KATIKA AJALI YA BOTI.

Makumi ya Waislamu wa Rohingya wafa maji katika ajali ya boti
CHANZO: PARSTODAY/SWAHILI
Kwa akali Waislamu 12 wa jamii ya Rohingya wamefariki dunia katika Mto Naf katika mpaka wa Myanmar na Bangladesh baada ya boti yao kuzama, wakikimbia mauaji na ukandamizaji unaofanywa na wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo dhidi ya jamii hiyo.
Kwa mujibu wa Luteni Kanali Ariful Islam, Kamanda wa Gadi ya Mpakani ya Bangladesh, boti hiyo iliyokuwa imebeba makumi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ilizama karibu na eneo la Shah Porir Dwip, katika mpaka wa nchi mbili hizo.

Amesema miili 12 ikiwemo 10 ya watoto wadogo na miwili ya watu wazima imepatikana katika operesheni ya usiku mzima na kwamba shughuli za kutafuta manusura na miili zaidi zingali zinaendelea.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, watoto 10 na wanawake wanne wa Rohingya walifariki dunia katika ajali nyingine ya kuzama boti katika mto huo, siku chache baada ya miili mingine 46 ya Waislamu wa Myanmar kupatikana katika tukio jingine la kuzama boti wakikimbilia usalama wao Bangladesh.
Hali ya kutisha ya wakimbizi Waislamu wa Rohingya.
Kwa mujibu wa takwimu mpya za Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, idadi ya wakimbizi wa jamii ya Rohingya waliokimbilia Bangladesh imepindukia laki 5 na elfu 50.
 
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema wakimbizi laki moja na nusu miongoni mwao wako katika hali mbaya na wanahitajia misaada ya dharura ya kibinadamu.

Waislamu hao wa Rohingya wamelazimika kukimbilia Bangladesh kutokana na mauaji na ukandamizaji wa jeshi la nchi hiyo likishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya jamii hiyo ya waliowachache katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.