ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 21, 2017

INGAWA MIGOGORO YA ARDHI MIJINI BADO MWIBA LAKINI NITAPAMBANA NAYO:- ASEMA MONGELA



NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGOBLOG

Migogoro ya ardhi katika sehemu za mijini bado zimekuwa mwiba kwa wananchi wengi kutokana na ongezeko la watu katika sehemu hizo.

Manispaa ya ilemela ni moja ya wilaya zinazokabiliwa na changamoto hiyo,ambapo mara kadhaa mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela ameingilia kati ili kutatua migogoro hiyo.

Ni mwezi mmoja na siku kadhaa zimepita tangu mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELA aliposikiliza na kutatua kero za ardhi zilizokuwa zikiwakabili wananchi wa wilaya ya Ilemela na Nyamagana mkoani mwanza.

Mongela akapata  fursa ya  kusikiliza kero za ardhi amabazo bado hazijatatuliwa tangu alipotoa maagizo kwa idara husika.

Mongela ameigeukia  idara ya ardhi na kuitaka kuunga jitihada za mkoa za kutatua migogoro na sio kuwa chanzo cha kuzalisha migogoro mingine.

Baadhi ya wananchi wameonekana kupongeza jitihada zinazo oneshwa na mkuu wa mkoa wa mwanza wa kusikilizana kutatua kero za ardhi ambazo zimekuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

Kikao hiki cha mkuu wa mkoa wa mwanza kimeweza kutatua migogoro kadhaa huku akitoa mwezi mmoja kwa idara ya ardhi ya wilaya ya ilemela pamoja na idara ya ardhi kanda ziwa kumaliza kabisa migogoro iliyosalia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.