Taarifa ya IEBC iliyosainiwa na Mwenyekiti, Wafula Chebukati
imesema uamuzi huo umefikiwa ili kuipa tume hiyo muda wa kujiandaa zaidi
na hasa katika masuala ya teknolojia.
Chebukati amesema kama tunavyomnukuu, “Ili kuhakikisha tume inajiandaa kuleta uchaguzi wenye viwango vinavyohitajika na Mahakama ya Juu, tunapenda kuujulisha umma na wadau wote kuwa uchaguzi mpya utafanyika siku ya Alkhamisi tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu 2017.”
Baraza la Mawaziri hapo jana liliidhinisha bajeti ya Shilingi bilioni 10 za Kenya zitakazotumiwa katika zoezi hilo.
Majaji wa Mahakama ya Juu Kenya
Mahakama ya Juu ya Kenya iliamuru uchaguzi wa marudio ufanyike ndani ya muda wa siku 60 kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa mrengo wa upinzani NASA Raila Odinga ambaye aliyapinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa Agosti 8 katika mahakama hiyo.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya ilikuwa imemtangaza Rais Kenyatta mshindi, kwa kumpiku Odinga kwa kura zaidi ya milioni moja na laki nne.
Rais Kenyatta na Odinga watakaochuana Oktoba 26

Uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Kenya kubatilisha ushindi wa rais
uliotangazwa tarehe Mosi ya mwezi huu wa Septemba ulikuwa wa kwanza
kutolewa barani Afrika na wa nne kote duniani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.