ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 15, 2017

OPARESHENI YA KUPAMBANA NA KIRUSI KINACHOSABABISHA ULEMAVU YAANZA TANZANIA.

Waratibu wa wilaya za mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa wametakiwa kuifikishia jamii mafunzo waliyopokea kwa takribani siku tatu juu ya kupambana na ugonjwa wa ulemavu wa ghafla unaosababishwa na kirusi hatari anaefahamika kwa jina la KIRUSIPOLI.

Agizo hilo limetolewa na Afisa mfuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo Honest Nyaki wakati akihitimisha mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku tatu mkoani njombe kwa waratibu wa wilaya ambayo yanalenga kuielimisha jamii jinsi ya kuepukana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Zoezi la utoaji mafunzo linafanyika nchi nzima kwa lengo la kutokomeza na kuelimisha jamii hasa katika kuwa na ufahamu juu ya magonjwa ya ulemavu wa ghafla ambao dalili yake kuu ni mwili kulegea na kuwa tepetepe dalili ambayo inatambulisha ugonjwa huo wa ulemavu wa ghafla ambao unasababishwa na kirusi kinachofahamika kama KIRUSIPOLI ( POLIO VIRUS ) kinachopatikana na kwenye kinyesi.

TAARIFA NA AMIRI KILAGALILA

POLIOVIRUS ndio jina halisi la kirusi hicho ambacho kwa lugha ya kiswahili kinafahamika kama KIRUSIPOLI , Kwa mujibu wa mtaalamu ambae ni afisa ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo anasema kuwa kirusi huyu ni hatari na amekuwa akiwakumba hasa watoto walio na umri chini ya miaka kumi na mitano .

CUE....................................................MTAALAMU.

Aidha jamii imetakiwa kuchukua hatua za haraka pindi wanapoona mtoto anadalili hiyo kuu mwili kulegea na kuwa tepetepe basi wachukue hatua za kuripoti katika vituo vya afya ili hatua za vipimo ziweze kufuata kwaajili ya matibabu ya mtoto.

CUE ......................................................WITO KWA JAMII.

Mwaka 1996 nchini tanzania mgonjwa wa ulemavu wa ghafla alipatikana kwa mara ya mwisho ambapo mpaka sasa hakujatokea tena mgonjwa au mwathirika wa ugonjwa huo hali ambayo imewalazimu watalaamu kuchukua hatua za kufanya uchunguzi kwaajili ya kutafuta kama ugonjwa huu upo ili kuweza kuuteketeza kabisa kwaajili ya usalama wa afya za watoto.

CUE............................................................UKUBWA WA TAITIZO LA ULEMAVU WA GHAFLA

Pius Willium Yonga na Dr.Huruma ni miongoni mwa waratibu ambao wamehudhuria katika mafunzo hayo ya siku tatu hapa mkoani njombe , ambao wanasema kuwa wameyapokea mafunzo kwa mikono miwili huku wakiahidi kuyapeleka mafunzohayo kwa jamii na kueleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kutokana na mpango uliopo wa kutokomeza magonjwa ya ulemavu wa ghafla pamoja na surua nchini tanzania.

CUE............................................................WARATIBU.

Hata hivyo jamii imetakiwa kuwa na matumizi sahihi ya vyoo bora ili kuhakikisha kuwa kirusi cha ugonjwa wa ulemavu wa ghafla hakipewi nafasi katika kuwadhuru watoto.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.