ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 1, 2017

WALIOFURUMISHA MAWE KWA MSAFARA WA MKUU WA WILAYA, WASAMEHEWA


 MKUU wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, amewasamehe wanakijiji wa Mlongia kata ya Jongolo waliobeba silaha za kijadi, virungu na mawe wakidaiwa kuupiga mawe msafara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo ulipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji hicho.

Akizungumza jana Jumatatu, Odunga amesema ameamua kuwasamehe na kutowafikisha mahakamani wakazi hao wanaodaiwa kuhusika katika vurugu hizo baada ya makubaliano kuwa hawatarudia tena kitendo kama hicho.

“Haina haja ya kuendelea na ugomvi na wananchi ambao unawaongoza.

Niliwasamehe na waliapa kutorudia tena vitendo kama hivyo na sasa hali imetulia,” amesema Odunga.

Tukio hilo lilitokea Januari mwaka huu wakati Kamati ya Ulinzi na

Usalama ya Wilaya hiyo ilipokuwa ikenda katika mkutano huo uliolenga

kujadili mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa kijiji hicho na mwekezaji

aliyetambulika kwa jina la Msukuma, ambaye anadaiwa kupewa ekari 500

kwa ajili ya kuwekeza katika eneo la kijiji hicho.

Kwa mujibu wa Odunga, hakuna haki ambayo imekiukwa na mwekezaji

huyo bali mvutano huo ulitengenezwa na wanasiasa.

“Hakuna haki ya msingi ambayo imekiukwa katika eneo hilo isipokuwa

mgogoro huo umesababishwa na elimu ndogo na wanasiasa  kuwachochea

wananchi,” alisema.

Alisema kimsingi shamba hilo la mwekezaji lenye ukubwa wa ekari 450 liko katika kijiji cha Kwadelo wilaya ya Kondoa na wala si wilaya ya Chemba.

“Na viongozi wa Wilaya ya Kondoa wanamtambua mwekezaji huyo lakini

wanasiasa hawa wamekuwa wakimpiga vita tangu mwaka 2006, sijui ni

kwa sababu gani,” alisema.

Katika tukio hilo, wanakijiji hao wakiwa na silaha za jadi, mapanga,

virungu na mishale walishambulia Kamati ya Ulinzi na Usalama na

kuharibu pia gari ya Mkuu wa Usalama wa Wilaya baada ya kulipiga mawe.

Tukio hilo lilisababisha watu 30 kukamatwa akiwemo mwenyekiti wa

kijiji na kuhojiwa kuhusiana na fujo hizo.a

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.