ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 1, 2017

"NAOGOPA AIBU, WATOTO WANGU NAWALEA KIJESHI" - MKUU WA MKOA WA MWANZA.



MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka walimu kuwa mfano wa malezi kwa watoto wao ili wazazi na jamii kwa ujumla wapate imani na ufundishaji wa walimu hao hasa pale wanapowakabidhi majukumu ya kuwalea watoto wao. 

Mongella aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifunga Mafunzo ya siku 9 kwa walimu wa wanafunzi viziwi na wasioona kwa darasa la 3 na la 4, yaliyofanyika Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza na kuhuduriwa na washiriki 294 wa mikoa mbalimbali hapa nchini. 

Alisema suala hilo haliishii tu kwa walimu hata viongozi nao wanadaiwa malezi bora kwa watoto wao kwani hata yeye amekiri kwamba anawalea kijeshi watoto wake ili kukwepa aibu kwa jamii.

"Nitawezaje kukemea au kupambana na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya ile hali, ikatokea hata mimi mwenyewe mtoto wangu akawa anavuta bangi?"
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Christopher mihayo mwalimu wa viziwi na wasioona kwa darasa la 3 na la 4 shule ya msingi mitindo wilayani Misungwi mkoani Mwanza akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, juu ya baadhi ya vitendea kazi na nyenzo za ufundishaji kwa wanafunzi husika wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya walimu.


Hivi ni vitendea kazi na nyenzo za ufundishaji kwa wanafunzi husika ili kutimiza malengo ya KKK (K3) Kusoma Kuandika na Kuhesabu ni mabanda ya maonesho ya walimu.
Yahitaji mifano katika ufundishaji na hizi ni baadhi ya nyenzo.
Timoth Paul Mwamba mwalimu wa wanafunzi wasioona na wenye uziwi toka Shule ya msingi Kizega Iramba mkoani Singida akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, juu ya baadhi ya vitendea kazi na nyenzo za ufundishaji kwa wanafunzi husika wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya walimu hao.
Yahitaji mifano katika ufundishaji na hizi ni baadhi ya nyenzo.
Ufundishaji usomaji wa ramani, hesabu alama za tarakimu vyote hivyo vinahitaji mifano ya vitu halisia katika ufundishaji na hizi ni baadhi ya nyenzo.
Suzan Emmanuel ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mwisenge, Musoma mjini mkoani Mara akitoa maelezo jinsi ya utambuzi wa saa na usomaji wake.
Suzan Emmanuel ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mwisenge, Musoma mjini mkoani Mara akitoa maelezo jinsi ya utambuzi wa samaki.
Kuku.
Zao la mpunga/mchele.
Awali kabla ya mafunzo haya ilionekana pengo kubwa kati ya ufundishaji kupitia mtaala wa zamani dhidi ya mtaala huu mpya wa sasa, ambapo wanafunzi wenye ulemavu wasioona na wenye uziwi walikuwa nyuma. "Ni matumaini ya Serikali kuwa baada ya mafunzo hayo pengo lililokuwepo litaondoka kabisa. Alisema Kasimu Kaoneka Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Rais inayoshughulikia elimu maalum. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA













Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.