Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe. |
Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akitoa maelekezo na ushauri. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Nicas Mayala akisisitiza kufanyia kazi ushauri ambao wamepatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
Baadhi ya wakuu wa Idara wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani Wilayani Bukombe. |
PICHA NA JOEL MADUKA
Halmashauri
zilizopo Mkoani Geita,zimetakiwa Kutangaza Vivutio ambavyo vitaweza kuwavutia
wawekezaji ili waweze kuwekeza kwenye
Maeneo yao.
Rai hiyo
ameitoa Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwenye
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe .
Ambapo
amesema kuwa Halmashauri Nyingi ikiwemo ya Bukombe ina maeneo mengi ambayo
yanauwezo wa kuwavutia wawekezaji tatizo kubwa ni kutokutangaza fursa hizo.
“Kwasababu
mwenye macho aambiwi tazama sisi wote jamani tunaona kwenye Vyombo vya habari
namna halmashauri mbali mbali zinavyochachalika kutangaza Fursa zao halmashauri
unakuta imejiwekea utaratibu inatangaza yenyewe fursa inaita wawekezaji mbali
mbali jamani ninachotaka kusema tuchachalike fursa tunazo na tuzitangaze tuone
ni wapi ambapo tunaweza kupata wawekezaji”Alisisitiza Kyunga.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Bukombe,Nicas Mayala amemwakikishia Mkuu wa mkoa kuanza
kufanyia kazi maelekezo na ushauri ambao ameutoa kwenye Halmashauri Hiyo huku
akiwataka wawekezaji kuja kuwekeza Bukombe kutoka na na kuwepo kwa mifugo mingi
ya Ng’ombe.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri Hiyo,Dionis Myinga amehaidi kufuatilia na kutafuta
wawekezaji ambao wataweza kuwekeza kwenye Wilaya Hiyo na kwamba bado kunafursa nyingi za uwekezaji .
Hatua hiyo
imekuja ni kutokana na halmashauri hiyo
,Mkoani Hapa Kuwa na Idadi Kubwa ya Mifugo ikiwemo Ng’ombe.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.